Deuteronomy 28:3-8

3 aUtabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani.

4 bUtabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ng’ombe, na wana-kondoo wa makundi yako.

5Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.

6

cUtabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.

7 d Bwana atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

8 e Bwana ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. Bwana Mwenyezi Mungu wako atakubariki katika nchi anayokupa.

Copyright information for SwhKC